Renson Mulele aapishwa kama mkurugenzi mkuu wa idara ya mashtaka ya umma katika ikulu ya Nairobi

  • | K24 Video
    38 views

    Renson Mulele Ingonga ameapishwa kama mkurugenzi mkuu wa idara ya mashtaka ya umma ambapo atahudumu kwa muda wa miaka minane. Jukumu kubwa linalomsubiri sasa ni kulinda uhuru wa idara hiyo na kukabiliana na ufisadi hususan miongoni mwa baadhi ya maafisa wakuu serikalini yeye ni wakili wa mahakama kuu na amekuwa akihudumu kama naibu mkurugenzi mkuu wa idara ya mashtaka ya umma katika eneo la kaskazini mashariki.