Reuben Kigame amshutumu Chebukati kwa kumtupa nje ya kinyang'anyiro cha urais

  • | Citizen TV
    651 views

    Mwaniaji wa urais kwa tikiti ya chama cha Federal Ruben Kigame anataka uchaguzi mkuu kuahirishwa akidai kuwa mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati hafai kuwa msimamizi wa tume hiyo. Kulingana naye, mwenyekiti wa IEBC alimpuuza bila ya kuzingatia sheria kwa kukosa kuchukua stakabadhi zake kabla ya kukataa kumuidhinisha kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao.