- 19,334 viewsDuration: 9:08Cheche za maneno, mirengo mipya ya kisiasa na ubabe wa vyama tayari imeanza kusheheni nchini Kenya, miezi 14 tu kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Miongoni mwa viongozi wanaogonga vichwa vya habari ni pamoja na aliyekuwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua aliyetimuliwa kazini miezi kadhaa iliyopita. Gachagua amekuwa akiendeleza kampeini ya kuunda muungano wa upinzani kwa nia ya kumng'oa madarakani Rais William Ruto. Gachagua amezungumza na BBC kuhusu azma yake ya kuwania urais... #DiraYaDuniaTV