Ripoti ya NACADA kuhusu utumizi wa pombe na mihadarati nchini

  • | K24 Video
    64 views

    Eneo la magharibi linaongoza kwa matumizi ya pombe na mihadarati kwa asilimia 23.8 ikifuatwa na pwani kwa asilimia 13.9% na Mlima Kenya ikifuata na asilimia 12.8%. hii ni kulingana na ripoti iliyozinduliwa hii leo na mamlaka ya kukabiliana na utumizi wa mihadarati (NACADA) inayoonyesha kuwa zaidi ya wakenya milioni 3 wanatumia mihadarati, cha kutamausha ni kuwa watoto wenye umri wa kati ya miaka sita na minane, wamefunzwa unywaji pombe na utumizi wa dawa za kulevya. Malezi mabaya na upatikanaji rahisi wa pombe umechangia pakubwa katika janga la uraibu wa mihadarati.