Royal Credit Ltd yazuia uuzaji wa hisa za Directline

  • | Citizen TV
    136 views

    Kampuni ya Royal Credit Limited inayomiliki hisa nyingi katika kampuni ya bima ya Directline Assurance imepinga hatua ya wanaodai kuwa wenye hisa katika kampuni hiyo ya kutaka kuuza asilimia 90 Ya hisa za kampuni ya Directline. Kupitia barua kwa mamlaka ya udhibiti wa bima ya IRA, Royal Credit Limited imesema, imeshangazwa kuona tangazo linaloashiria azma ya kuuza asilimia 90 ya hisa ilihali mmliki mwenye hisa nyingi katika kampuni ya Directline, Royal Credit haijatoa kibali au kutangaza haja ya kuuza hisa. Royal Credit imetahadharisha wateja dhidi ya kupunjwa au kuingia kwenye mtego wa ufisadi wa kununua hisa ambazo si halali. Sasa inaitaka mamlaka ya IRA kuthibitisha iwapo imepokea barua bandia kuhusu uuzaji wa hisa. Pia imesisitiza kuwa uuzaji wa hisa zozote unastahili kuidhinishwa na wenye hisa wake pekee.