Rais William Ruto ametia saini Mswada wa Hazina ya Rasilimali za Taifa kuwa sheria, hatua inayolenga kuweka mfumo wa ukusanyaji na usimamizi wa mapato yatokanayo na rasilimali kama madini na mafuta.
Sehemu ya fedha hizo itaelekezwa katika uwekezaji wa miradi ya maendeleo, huku nyingine ikiwekwa akiba kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Rais amesema sheria hiyo itasaidia kuhifadhi utajiri wa Kenya na kuhakikisha mapato yanayotokana na rasilimali za taifa yananufaisha vizazi vya sasa na vijavyo.
Viongozi waliohudhuria hafla hiyo walimuunga mkono Rais na kumtaka kupuuza wakosoaji, wakisema anapaswa kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kwa manufaa ya taifa.