Ruto : Mkumbatie mfumo wa E-Procurement au mjiondoe serikalini

  • | KBC Video
    340 views

    Rais William Ruto amesema hatalegeza kamba katika utekelezaji wa mfumo wa utoaji zabuni kielekroniki almaarufu E-procurement serikalini akisema kwamba hatua hiyo itapiga jeki vita dhidi ya ufisadi na ubadhirifu wa rasilimali za umma. Katika kile kinachokisiwa kuwa majibu kwa wabunge na magavana wanaopinga utekelezaji wa agizo hilo, rais Ruto alionya wale ambao hawako tayari kukumbatia mfumo huo kujiondoa serikalini. Haya yanajiri huku kiongozi wa taifa akisema serikali haitalipa deni la shilingi bilioni-30 ambazo iliyokuwa hazina ya kitaifa ya bima matibabu –NHIF ilikuwa inadaiwa hadi litakapohakikiwa. Mwanahabari wetu Abdiaziz Hashim na uketo wa taarifa hii.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive