Ruto : Serikali kuboresha makazi kwenye mitaa ya mabanda

  • | KBC Video
    40 views

    Rais William Ruto amesema atajizatiti kuhakikisha kwamba Wakenya wanaoishi katika mitaa 1,400 ya mabanda wamepata makazi ya kudumu. Akiongea katika Ikulu ya Nairobi wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya mpango endelevu wa ustawishaji miji, rais alisema mpango huo umewadia kwa wakati ufaao na utashughulikia tatizo la mitaa ya mabanda ikizingatiwa kwamba miji imeathiriwa pakubwa na mabadiliko ya tabianchi. Rais alisema mpango huo utakaogharimu dola milioni 350 utatekelezwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo na utatoa suluhu kwa tatizo la mafuriko yanayoshuhudiwa humu nchini.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive