Ruto: Sitishwi na vitisho vya ‘wantam’, nitaendeleza maendeleo

  • | Citizen TV
    1,838 views

    Rais william ruto amewakashifu viongozi wa upinzani akiwaonya dhidi ya kumrushia vitisho vya kuwa rais wa muhula mmoja pekee. Akihudhuria ibada ya jumapili katika eneo bunge la Limuru kaunti ya Kiambu, Rais Ruto ambaye baadaye alizuru mradi wa nyumba za serikali eneo hilo alisema ana mpango bora wa maendeleo kwa wakenya. Gavana wa kaunti hiyo kimani wamatangi akitaka wenyeji kuweka kando siasa kwa sasa na kuungana na rais ruto kufanya maendeleo.