Safari ya Kaa ya kila mwaka yaanza nchini Australia

  • | BBC Swahili
    538 views
    Kila mwaka, makumi ya mamilioni ya kaa wekundu huvamia Kisiwa cha Krismasi cha Australia, kilicho kilomita 2,600 kutoka Perth katika Bahari ya Hindi. Kaa hufanya hija yao ya kila mwaka kutoka kwenye uwanda wa msitu hadi baharini ili kujamiiana na kuzaa. Uhamiaji wa kila mwaka huanza na mvua ya kwanza ya msimu wa mvua. Sio tu tukio kuu kwa kaa, lakini pia kwa wakazi wa visiwani - wakati trafiki inapoelekezwa kuwalinda kaa wanaoweka zulia barabarani. #bbcswahili #wanyama #australia