Sakata ya elimu ya Finland

  • | Citizen TV
    2,154 views

    Kwa wiki kadhaa sasa, sakata ya ulaghai wa mamilioni ya pesa kwenye mpango wa masomo ya Finland na Canada imegongwa vichwa vya habari kufuatia malalamishi kutoka kwa mamia ya wazazi na wanafunzi. Kulingana na wazazi hao miaka miwili baada ya kuagizwa kutoa zaidi ya milioni moja kila mmoja kuwawezesha watoto wao kusomea mataifa hayo bado watoto wao wanahangaika huku wakisalia wachochole baada ya kuuza mali yao. Runinga ya Citizen imefuatilia namna mpango huo ulivyoanzishwa na kuwafaidi zaidi ya wanafunzi 200 kabla ya ufujaji wa pesa kuanza kugubika mpango huu mwaka jana.