Salasya Mashakani I Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya amulikwa na tume ya maadili-EACC

  • | KBC Video
    158 views

    Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya amejipata kwenye mkono mbaya wa sheria baada ya kuagizwa kufika mbele ya tume ya maadili na vita dhidi ya ufisad-EACC. Salasya anamulikwa na tume ya EACC kwa madai ya kukiuka sura ya sita ya katiba kwa kumshambulia hadharani mwakilishi wadi ya Malaha-Isongo-Makunga Peter Walunya Indimuli wakati wa ibada ya mazishi katika eneo la Mumias Mashariki kaunti ya Kakamega. Afisa mkuu wa tume ya EACC Twalib Mbarak amesema madai dhidi ya Salasya yanahusisha masuala mazito ya kimaadili na iwapo yatathibitishwa basi huo ni ukiukaji mkubwa maadili kwa maafisa wa serikali. na jinsi anavyotaarifu Abdiaziz Hashim, Salasya ameagizwa kufika katika afisi za tume ya EACC mnamo Jumanne wiki ijayo kuandikisha taarifa.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News