sarafu za kidijitali zinafanya kazi vipi?

  • | BBC Swahili
    588 views
    Mamlaka nchini Nigeria zimeshutumu kampuni ya sarafu za kidijitali ya Binance kwa kujishughulisha na utakatishaji wa fedha. Aidha mmoja wa wakurugenzi katika kampuni hiyo aliyekuwa amekamatwa mwezi uliopita sasa anasakwa na polisi baada ya kutoroka kizuizini. Binance imesitisha shughuli za kibiashara kupitia sarafu ya Naira ya Nigeria. Katika miaka ya hivi karibuni, sarafu za kidijitali maarufu kama 'Cryptocurrency' zimekuwa zikipata umaarufu duniani na barani Afrika. Nigeria ni taifa lenye matumizi makubwa zaidi ya sarafu hizi barani Afrika. Lakini sarafu hii inafanya kazi vipi? Leila Mohammed anaelezea. #bbcswahili #nigeria #sarafukidigitali Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw