Seneta Omtatah awasilisha kesi mahakamani

  • | Citizen TV
    1,684 views

    Seneta wa Busia Okiya Omtatah, anataka sheria mpya ya nyumba kutupiliwa mbali na mahakama, kwa kuwa inabagua jukumu la utoaji ushuru miongoni mwa walioajiriwa na wasiokuwa na ajira. Aidha, kiongozi huyo pamoja na walalamishi wengine watatu wanadai kwamba sheria hiyo itatumika kutekeleza ufisadi wa fedha ambazo zitakazokusanywa kupitia utoaji ushuru.