Skip to main content
Skip to main content

Sera ya mwongozo wa kusaidia waathiriwa wa dhuluma za kijinsia yazinduliwa Tana River

  • | Citizen TV
    86 views
    Duration: 1:46
    Ni afueni kwa waathiriwa wa dhuluma za kijinsia baada ya serikali ya kaunti ya Tana River pamoja na mashirika ya kijamii kuzindua sera itakayotoa mwongozo wa jinsi waathiriwa wa dhulma hizo watakavyo shughulikiwa kisheria. Akizindua sera hiyo mjini Hola, Waziri wa jinsia katika kaunti ya Tana River Abass Kunyo alisema sera itahakikisha kuwepo kwa kituo cha kuwasaidia manusura wa dhulma za kinjisia na wahusika kukabiliwa vilivyo kisheria. Aidha sera hii inatarajiwa kushinikiza bunge la kaunti hiyo kutenga fedha za kufanikisha ajenda hiyo.