Serikali imeanza kuwaondoa wanaoishi karibu na mito

  • | Citizen TV
    348 views

    Serikali imeanzisha mchakato wa kuwaondoa watu wanaoishi karibu na mito ya Ngong, Nairobi na Mathare ili kuboresha mazingira ya mito hiyo inayopitia ndani ya jiji la Nairobi. Akizungumza na tume ya kusimamia mito hiyo katika ofisi yake iliyoko Karen, naibu wa Rais Rigathi Gachagua amesema kuwa uchafuzi wa mito hiyo ni hatari kwa afya ya wakazi wa Nairobi na hivyo ni lazima isafishwe.