Serikali inasema inachunguza kupotea kwa umeme

  • | Citizen TV
    3,479 views

    Serikali inaendeleza uchunguzi kuhusu chanzo cha taifa kukosa umeme tangu siku ya ijumaa. Katibu wa wizara ya kawi alex wachira amesema uchunguzi huu unaendelea huku vita ni kuvute ikiendelea kuhusu ni nani wa kulaumiwa kwa kupotea kwa umeme nchini. Ingawa wizara ya kawi ilikuwa imelaumu kituo cha umeme wa upepo cha turkana kwa yaliyojiri, kituo hicho kimeshikilia kuwa hakina lawama yoyote.