Serikali inasema ni watu 51 pekee walioidhinishwa kusafiri Dubai kwa kongamano la COP28

  • | Citizen TV
    238 views

    Serikali sasa inasema ni watu 51 pekee walioidhinishwa kwenye ujumbe wake ulioelekea mjini Dubai kwa kongamano kuhusu mabadiliko ya hali ya anga ya COP28. Msemaji wa ikulu Hussein Mohammed amekana ripoti zilizoashiria idadi kubwa ya maafisa wanaowakilisha Kenya kwenye kongamano hilo linaloendelea kwenye himaya ya milki za kiarabu. Hussein alikuwa akizungumza kwenye mahojiano na runinga ya Citizen jana usiku