Skip to main content
Skip to main content

Serikali kugharamia matibabu ya manusura wa ajali ya Webuye na gharama ya mazishi kwa waliofariki

  • | Citizen TV
    277 views
    Duration: 2:11
    Majeruhi wawili wa ajali ya trela iliyowauwa watu kumi na watano katika eneo la Malaha huko webuye wamehamishwa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Webuye ili kupokea matibabu maalum. Akizungumza baada ya kutembelea familia za waathiriwa, Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula aliahidi kuwa serikali itagharamia matibabu ya majeruhi 10 pamoja na gharama ya mazishi ya watu 15 waliopoteza maisha katika ajali hiyo. Ibada ya wafu ya pamoja imepangiwa kufanyika Jumatatu wiki ijayo mjini Bungoma. Aidha familia za waathiriwa zinadai haki zikitaka asasi za usalama kuhakikisha kuwa waliosababisha ajali hiyo wamekamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.