- 736 viewsDuration: 2:52Itailazimu serikali na sekta ya kibinafsi kushirikiana kwa ujenzi wa vituo vya wasafiri katika Barabara kuu nchini, kama njia ya kuwasaidia wasafiri kupata vyoo, na pia kuwaepusha na magonjwa. Hili litategemea kuidhinishwa mswada uliowasilishwa na seneta wa Nyeri Wahome wamatinga ambao unaoshinikiza ujenzi wa vituo hivyo.. Seneta huyo anasema mswada utakapopitishwa, vituo hivyo vitakuwa vikijengwa wakati wa ujenzi wa Barabara zozote kuu.