Serikali kumfanyia kampeni kiongozi wa upinzani Raila kuwania kiti cha muungano wa Afrika

  • | K24 Video
    1 views

    Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amepongeza hatua ya serikali ya kumuunga mkono na kumsadia katika kufanya kampeni ya kuwania uenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika, AUC. akizungumza hii leo na wanahabari katika kikao cha pamoja na mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi,odinga amesema kuwa kuungwa mkono na serikali kunapiga jeki kampeni yake na hivyo hakuna kinachomzuia kushinda kiti hicho. Serikali imebuni sekretarieti ya kumfanyia Odinga kampeni.