Serikali kuwasilisha neti za kuzuia mbu Nyamira

  • | Citizen TV
    755 views

    Katibu wa Wizara ya Afya nchini Mary Muthoni ameongoza hafla ya kuandikisha wananchi kupokea neti za kuzuia mbu wanaosababisha malaria katika kaunti ya Nyamira. Kama njia moja ya kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa malaria nchini, serikali kwa ushirikiano na wafadhili wengine ina mpango wa kuwasilisha neti milioni 15.3 katika kaunti 22, huku kaunti ya Nyamira inatarajia kupokea zaidi neti zaidi ya laki tano nayo kaunti jirani ya ya Kisii ikitarajiwa kupokea zaidi ya neti 900,000. Usajili huo unatarajiwa kukamilika hii leo katika kaunti hiyo ya Nyamira ambapo zaidi ya asilimia tisaini ya wananchi wamesajiliwa.Katibu huyo amewashauri wananchi kuchukua bima ya afya ili kugharamia matibabu katika hospitali za umma kote nchini.