Serikali ya kaunti ya Kajiado yapiga marufuku shughuli zote kwenye ardhi ya Oldonyonyokie

  • | Citizen TV
    202 views

    Siku moja baada ya Wanachama wa Kundi la Oldonyonyokie, huko magadi kaunti ya kajiado kulalamikia njama ya ardhi yao kunyakuliwa na watu ambao si wanachama wa kundi hilo la malisho, Serikali ya kaunti ya Kajiado kwa ushirikiano na bodi ya ardhi kaunti hiyo imepiga marufuku shughuli zote kwenye ardhi hiyo hadi tarehe 19 mwezi ujao wakati ambapo mkutanao wa wanachama utaandaliwa.Akitoa Tangazo hilo baada ya mkutano na bodi hiyo, Gavana wa Kajiado Joseph Ole Lenku anasema hatua hiyo itatuliza hofu iliyokuwepo na kutoa nafasi kwa wanachama kuamua njia ya kugawanya ardhi hiyo.