- 191 viewsDuration: 1:37Serikali ya kaunti ya Kilifi imewataka manesi ambao wako kwenye mgomo kurudi kazini Mara moja, ikionya kwamba huenda ikawachukulia hatua kwani mgomo wao haufuati sheria. Waziri wa Afya kaunti ya Kilifi Peter Mwarogo anasisitiza kuwa mgomo wa manesi hao si halali kwani matakwa yao yamekuwa yakitekelezwa Mara kwa Mara na serikali ya kaunti hiyo. Msemaji wa serikali ya kaunti ya Kilifi Jonathan Mativo ametoa wito kwa manesi hao kufanya mazungumzo na serikali ili kupata mwafaka kuhusu mgomo huo.