Serikali ya kaunti ya Kisii yazindua mpango wa kusambaza dawa

  • | Citizen TV
    140 views

    Serikali ya kaunti ya Kisii imeanzisha mchakato wa kuongeza dawa katika hospitali mbalimbali kaunti hiyo kama njia moja wapo ya kupiga jeki sekta hiyo ya afya. Uzinduzi wa mpango huo unaofanyika katika hospitali ya rufaa ya Kisii ukiongozwa na gavana wa kaunti hiyo Simba Arati unanuiwa kuziba mianya ya wizi wa dawa hizo ambao umekuwa changamoto kubwa kwa muda.