Serikali ya kaunti ya Siaya yaanzisha miradi ya unyunyizaji wa maji mashambani

  • | Citizen TV
    107 views

    Serikali ya kaunti ya Siaya imeanzisha mradi wa unyunyizaji maji mashamba katika eneo la Lower Nzoia ambao unatarajiwa kukamilika Mwezi Septemba na kuimarisha kilimo cha mpunga katika eneo la Usonga. Mbali na hayo mipango ya kuharakisha ujenzi wa kiwanda cha mpunga inaendelea ili kuhakikisha kaunti hiyo inafaidika na kilimo hicho. Gavana James Orengo ameeleza kuwa hiyo ndio mbinu ya kuhakikisha kuwa bidhaa za kaunti ya Siaya zinafikia viwango vya soko humu nchini na kushindana na kaunti zingine zinazojihusisha na kilimo na uzalishaji.