Serikali ya kaunti ya Tharaka Nithi yapiga jeki wakulima wa kahawa

  • | Citizen TV
    362 views

    Serikali ya Tharaka Nithi inapania kufufua kilimo cha kahawa ili kumpa mkulima mapato zaidi. Akizungumza na wadau wa sekta hiyo mjini Chuka, gavana wa kaunti hiyo Muthomi Njuki amemewaeleza kuwa serikali yake ina mpango wa kutoa mafunzo na baadaye miche kwa wakulima. Wakulima wengi wa zao hilo waligeukia ukulima wa mimea mingine kama mahindi kutokana na mapato duni. Sasa wanahimizwa kupanda mibuni kwani kahawa ya kenya ina soko kubwa ughaibuni.