Serikali ya kaunti ya Uasin Gishu imewasimamisha kazi maafisa waliowapeleka wanafunzi Finland

  • | K24 Video
    137 views

    Serikali ya kaunti ya uasin gishu imewasimamisha kazi maafisa wake waliohusika katika sakata ya kuwapeleka wanafunzi katika taifa la Finland. Wanafunzi hao wanakabiliwa na hatari ya kufurushwa katika vyuo walivyojiunga navyo baada ya pesa waliolipa kudaiwa kufujwa na watu fulani. Gavana wa Uasin Gishu Jonathan Bii ametangaza kwamba serikali yake imesitisha shughuli zote za kupeleka wanafunzi katika mataifa ya kigeni huku uchunguzi wa sakata hiyo ukiendelea.