Serikali ya Kenya Kwanza imeanzisha rasmi jitihada za kuhalalisha makato ya nyumba za bei nafuu

  • | K24 Video
    79 views

    Serikali ya Kenya Kwanza imeanzisha rasmi jitihada za kuhalalisha makato ya nyumba za bei nafuu yaliyoharamishwa na mahakama kuu hivi majuzi. Kupitia kiongozi wa wengi bungeni Kimani Ichungwa, serikali imewasilisha mswada unaolenga kutekeleza ibara ya 43 ya katiba; kutoa mfumo wa upatikanaji wa nyumba za bei nafuu na kwa madhumuni yanayofungamana na shughuli hiyo. mswada huo unapendekeza bodi isimamie fedha hizo.