- 144 viewsDuration: 2:05Serikali ya Kaunti ya Machakos kwa kushirikiana na Mtandao wa Afrika wa Ustawi wa Wanyama (ANAW) imeanzisha mpango wa kuwachanja mbwa na paka wote katika Wadi ya Kivaa katika kaunti ndogo ya Masinga dhidi ya kichaa cha mbwa.. Hatua hii imechukuliwa baada ya mlipuko wa kichaa cha mbwa ambapo watu 7 waliumwa na mbwa wenye kichaa katika Soko la Kivaa wiki moja iliyopita. Zoezi hilo lilianza Jumatatu katika vijiji 15 kati ya vijiji 34 vya kata nzima ya Kivaa na linaendelea.