Serikali ya Trans Nzoia yaonya mashirika ya mikopo dhidi ya kuwanyanyasa waendeshaji bodaboda

  • | Citizen TV
    208 views

    Serikali ya Kaunti ya Trans Nzoia imetoa onyo kwa mashirika yanayotoa mikopo ya bodaboda kutotumia vibaya leseni za kutoa huduma na kuwalaghai waendeshaji bodaboda kaunti hiyo. Akizungumza katika hafla ya kutoa fursa kwa wahudumu wa bodaboda kupata mikopo ya pikipiki mpya, waziri wa biashara wa kaunti ya Trans Nzoia, Patrick Gacheru, amesema hawatasita kuwachukulia hatua mashirika yatakayokuwa yanawanyanyasa waendeshaji bodaboda. Haya yanajiri huku takwimu kutoka Idara ya Biashara zikionyesha kuwa sekta ya bodaboda imeajiri zaidi ya watu 80,000, na inachangia pakubwa nafasi za ajira miongoni mwa vijana