Skip to main content
Skip to main content

Serikali yaagiza taarifa za watoto waliopotea zitolewe mara moja

  • | Citizen TV
    204 views
    Huku wasiwasi ukizidi kuibuliwa kuhusu idadi ya watoto wanaoripotiwa kutoweka kila siku nchini, Waziri wa Jinsia na Watoto, Hannah Cheptumo Wendot, ameamrisha kuwa kesi zinazohusu watoto waliopotea ziripotiwe mara moja badala ya kusubiri hadi saa 24 kama ilivyokuwa awali. Takwimu zinaonyesha kuwa watoto 23 hupotea kila siku, huku zaidi ya elfu kumi wakiripotiwa kutoweka tangu Januari mwaka jana hadi sasa. Wazazi waliopoteza watoto wao na bado hawajawapata wametakiwa kuzuru vituo vya serikali ambavyo vinawahifadhi zaidi ya watoto elfu 44 ambao wazazi wao hawajatambuliwa. Willy Lusige anaarifu zaidi.