Serikali yahimizwa ipige marufuku chupa za plastiki

  • | K24 Video
    77 views

    Wadau wa mazingira na sekta ya utalii wameishinikiza serikali ipige marufuku chupa za plastiki kama njia moja wapo ya kuboresha mazingira salama baharini. Wadau hao wameeleza kughadhabishwa kwao na ongezeko la taka za plastiki baharini ambazo ni hatari kwa viumbe vya baharini, watu na mimea inayopatikana katika fuo za bahari.