Skip to main content
Skip to main content

Serikali yahimizwa kuandaa mabaraza ya wananchi ili kuwapa nafasi ya kuchangia maendeleo

  • | Citizen TV
    139 views
    Duration: 1:41
    Serikali za kaunti zimetakiwa kukumbatia mfumo wa Mabaraza ya Wananchi kama njia moja kuu ya kuhakikisha wapiga kura wanahusika kikamilifu katika mipango ya maendeleo. Mashirika ya kiraia nchini yakiongozwa na Chama cha Kitaifa cha Walipa Kodi (NTA ) yamesisitiza umuhimu wa serikali za kaunti kuhakikisha wananchi wanapokea hamasisho kuhusu usimamizi wa fedha za umma ili waweze kushiriki kikamilifu katika maamuzi yanayohusu matumizi ya rasilimali za umma. Wakizungumza huko Nandi waakilishi wa mashirika hayo wamesema mabaraza haya yatawapa wananchi nafasi ya kuwauliza maswali maafisa wa serikali na kudai huduma bora kama vile maji, barabara, na afya.