Serikali yahimizwa kuhakikisha upatikanaji wa sodo

  • | KBC Video
    0 views

    Mashirika ya kutetea haki za wasichana katika kaunti ya Kilifi yamehimiza serikali kubuni mikakati ya kudumu na kuhakikihsha mradi wa utoaji sodo kwa wanafuzi wa kike shuleni unadumishwa . Kulingana na wadau hao, wasichana wengi katika eneo hilo wanaishi maisha ya uchochole, na upatikanaji wa sodo kwao ni changamoto. Wakizungumza katika warsha ya kujadili changamoto zinazowakumba wasichana mjini Kilifi,washikadau hao wamekashifu tetesi za kusitishwa kwa mradi huo wakidai kuwa ukosefu wa sodo umechangia ongezeko la visa vya dhuluma za kijinsia miongoni mwa wasichana. Wakiongozwa na shirika la Akili dada, washikadau hao wamesema ipo haja ya serikali kuweka sheria kali na kuwaadhibu wanaotekeleza dhuluma hizo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive