Serikali yahimizwa kuwajumuisha vijana katika miradi

  • | KBC Video
    26 views

    Viongozi wa kidini na kijamii katika kaunti ya Kisumu wanaitaka serikali ya kitaifa na serikali ya kaunti hiyo kutilia maanani miradi inayowalenga vijana ili kukabiliana kikamilifu na ongezeko la visa vya uhalifu hususan katika mitaa ya mabanda.Mwenyekiti wa Baraza la kitaifa la makanisa humu nchini askofu Clement Otieno na mwenzake wa baraza la waislamu sheikh Juma Kamsur walisema kuwa ukosefu wa fursa za kujiendeleza umewapotosha vijana humu nchini wanaogeukia shughuli za uhalifu ambazo zinaibua taharuki miongoni mwa wakazi wa kaunti hiyo .Viongozi hao wanahimiza kuwepo kwa mipango madhubuti ya kukabiliana na uraibu wa dawa za kulevya miongoni mwa vijana

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive