Serikali yasema imesambaza Ksh. 10b kwa kaunti kushughulikia athari za mafuriko

  • | Citizen TV
    1,371 views

    Naibu rais Rigathi Gachagua amewataka magavana kutumia fedha zilizotengewaudhibiti wa mafuriko kuweka mikakati ya kuhakikisha miundomsingi ya kupitisha maji iko shwari na kuwapa misaada waathiriwa. akizungumza huko mombasa, gachagua amesema kuwa serikali tayari imetoa shilingi bilioni kumi kwa serikali za kaunti ili kukabili athari za mafuriko. Gachagua amekanusha kauli ya gavana wa mombasa abdulswamad Shariff kuwa haijatoa msaada wowote kwa waathiriwa wa mafuriko. Gachagua amesema kuwa athari za mafuriko mombasa zimechangiw ana gavana kutojipanga.