Serikali yasema itanunua vifaa vya kisasa vya usalama kwa shilingi bilioni 37

  • | Citizen TV
    674 views

    Serikali itatumia kima cha shilingi bilioni 37 katika muda wa miaka mitano kununua vifa vya kisasa vya usalama ili kuwawezesha maafisa wa usalama kupambana na uhalifu, ikiwemo ugaidi, wizi wa mifugo na ulanguzi wa mihadarati. Akizungumza katika kaunti ya Lamu, waziri wa Usalama wa ndani Prof Kithure Kindiki amesema tayari awamu ya kwanza ya vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi bilioni saba vimewasili humu nchini na vitapokezwa wakuu wa vitengo vya usalama katika muda wa wiki moja.