Serikali yasema shule zitafunguliwa wiki ijayo

  • | Citizen TV
    2,129 views

    Huku mafuriko yakizidi kusababisha maafa na mahangaiko nchini, Naibu Rais Rigathi Gachagua amesema kwamba ufunguzi wa shule kwa muhula wa pili utaendelea kama ilivyoratibiwa licha ya jumla ya shule 64 kuathiriwa na mafuriko nchini. Aidha, naibu rais amesema kuwa serikali itatathmini hali na kutoa mwelekeo kuhusu athari za mafuriko kwa shughuli za masomo. Gachagua amesema kuwa serikali kuu iko tayari kushirikiana na zile za kaunti ili kutatua changamoto zinazotokana na mafuriko