Skip to main content
Skip to main content

Serikali yataja kaunti 12 hatarini kupata Ebola

  • | Citizen TV
    546 views
    Serikali imetangaza kaunti 12 nchini kuwa katika hatari kubwa zaidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Ebola. Katibu wa Afya ya Umma, Mary Muthoni amesema kuwa licha ya kutokuwepo kwa kisa chochote kilichothibitishwa nchini, serikali tayari imepima sampuli 22 za visa vinavyoshukiwa kuwa vya Ebola. Haya yanajiri saa chache baada ya Uganda kuthibitisha visa sita vipya vya Ebola, na kufikisha jumla ya maambukizi kuwa watu 15.