Serikali yatakiwa kukinga sekta ya nguo kupitia kilimo cha pamba

  • | KBC Video
    28 views

    Wakulima wea pamba katika eneo la Yatta wametoa wito kwa serikali kukinga sekta ya nguo humu nchini kama sehemu ya kuhimiza matumizi ya bidhaa zilizotengenezewa humu nchini. Wakulima hao wanasema kufanya hivyo kutawawezesha vijana kupata ajira.Walisifia hatua ya hivi majuzi ya kuongezwa kwa bei ya pamba kutoka shilingi 52 hadi shilingi 72 kwa kilo wakisema itawashawishi wakulima zaidi kukumbatia kilimo cha pamba. Wakiongozwa na David Kioko kutoka eneo la Ndalani, wakulima hao waliokusanyika katika kiwanda cha pamba cha Thika walitoa wito kwa serikali kuunga mkono uhuishaji wa sekta ya pamba kama sehemu ya kupiga jeki uchumi wa taifa hili.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive