Serikali yatakiwa kuwekeza katika vifaa vya kudhibiti majanga

  • | Citizen TV
    209 views

    Serikali kuu, serikali za kaunti kote nchini, taasisi za umma pamoja na kampuni zimetakiwa kuwekeza katika mikakati ya kupambana na majanga hasa moto ili kuzuia uharibifu wa mali panapotokea mikasa. Wadau katika sekta ya usalama na majanga nchini wamedokeza kuwa mikasa mingi iliyoripotiwa inaweza kuepukika iwapo wafanyakazi wanaweza kupewa mafunzo pamoja na kuwekeza katika vifaa vya kukinga au kukabiliana na Mikasa.