Serikali yatangaza fidia kwa familia zilizoathiriwa na uvamizi wa wanyama pori

  • | KBC Video
    27 views

    Familia elfu-7 zilizoathiriwa na uvamizi wa wanyama pori zinatarajia kufidiwa shilingi bilioni-3 katika muda wa miezi miwili ijayo. hatua hii inafuatia agizo la rais William Ruto alipokuwa akizindua mpango wa fidia kwa wahanga wa mashambulizi ya wanyama pori katika eneo la Rumuruti, kaunti ya Laikipia. Aidha, rais Ruto alitangaza kuwa mipango inaendelea ya kuweka ua wa kielektroniki kwenye eneo la kilomita-350 kuzingira mbuga na hifadhi za wanyama pori katika kaunti 6 ili kuzuia mizozo kati ya binadamu na wanyama pori.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News