Serikali yatetea mpango wa kuondoa chakula bila malipo kwa Wanajeshi

  • | Citizen TV
    613 views

    SERIKALI IMETETEA HATUA YAKE YA KUFUTILIA MBALI CHAKULA CHA MCHANA CHA BILA MALIPO KWA WANAJESHI. WAZIRI WA ULINZI SOIPAN TUYA AMESEMA KUWA SERIKALI IMEWAONGEZEA MARUPURUPU WANAJESHI ILI KUWAWEZESHA KULIPIA VYAKULA HIVYO KAMBINI. TUYA AIDHA ALISEMA WANAJESHI AMBAO WAKO KWENYE MAENEO YA OPERESHENI WANAENDELEA KUPATA VYAKULA HIVYO BILA MALIPO YOYOTE AKISISITIZA HATUA ILIYOCHUKULIWA KUANZIA MWEZI JULAI ITAIMARISHA CHAKULA CHA WANAJESHI WA KDF