- 1,178 viewsDuration: 5:13Serikali imethibitisha kuwa mkenya mmoja aliuawa nchini Tanzania wakati wa machafuko ya baada ya uchaguzi nchini humo. Katibu wa wizara ya usalama Raymond Omollo, aidha amesema serikali inafanya uchunguzi wa kina ili familia ya marehemu John Okoth Ogutu, aliyekuwa akifanya kazi tanzania kama mwalimu inapata haki. Wakati huo huo, serikali imewahimiza wakenya walio na jamaa zao tanzania kuandikisha jamaa zao.