- 248 viewsDuration: 1:53Serikali imezindua rasmi zoezi la usambazaji wa dawa ya kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV Lenacapavir (Lenacapavia) hii Leo. Akizingumza wakati wa kikao hicho katika kituo cha afya cha Riruta Health Center kilichoko mtaa wa Kawangware jijini Nairobi, Waziri wa afya Adeb Duale alisema kuwa hii ni hatua kubwa katika vita dhidi ya ugonjwa wa ukimwi. Duale amesema kuwa dawa hiyo itapeanwa katika vituo vilivyoidhinishwa bila malipo akiwaonya wenye njama ya kuwatapeli wakenya.