- 287 viewsDuration: 2:48Maelfu ya walimu wa Chama cha KUPPET wamepata afueni baada ya Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA) kuweka kiwango cha malipo ya huduma za hospitali kutoka shilingi 1,200 hadi shilingi 10,000 kila mara wanapoenda hospitalini. Akizungumza mjini Naivasha, Waziri wa Afya Adan Duale amesema kuwa mamlaka ya SHA imejadiliana na walimu na kutatua changamoto walizokumbana nazo wakitafuta huduma hospitalini.