Shabiki wa DRC avutiwa na mchezo walio uonyesha Leopards

  • | VOA Swahili
    276 views
    Fidel, shabiki wa timu ya Leopards ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo asema amefurahishwa na mchezo walioonyesha timu yake katika Kombe la Mataifa ya Afrika, licha ya kupoteza ushindi kwa penalti ya mabao 6-5 kwa timu ya Afrika Kusini ya Bafana Bafana katika nafasi ya tatu. Akiongea na VOA, Fidel alisema Leopards waliweza kuleta furaha kwa taifa la Afrika ya Kati ambapo mapigano yanaendelea kati ya majeshi yanayo unga mkono serikali na waasi wa M23. “Kama unavyojua, huko DRC hakuna kinachoenda vizuri. Umewaona vijana wetu wakati wa nusu fainali. Walikuwa wamevaa bendera nyeusi kuonyesha kuwa wao wanatokea Conga na hapa ( Ivory Coast) wanaungana na baba, mama na kaka zetu huko DRC ambao wamepoteza familia zao,” alisema. #afcon #totalenergiesafcon2023 #soccer #football #africa #news #voaafrica⁣