Shambulizi la Israel laharibu jengo, mwanafunzi aeleza hofu iliyowagubika

  • | VOA Swahili
    278 views
    Syria imesema Jumatano kuwa mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Israeli yamepiga makazi ya raia huko Damascus, na kuua watu wasiopungua wawili. Shirika la Habari la Syria lilisema mashambulizi hayo yamefanyika katika kitongoji cha Kfar Sousseh, ambacho ni makao makuu ya usalama na jeshi. Hakuna maelezo ya haraka kuhusu shambulizi hilo kutoka kwa jeshi la Israeli, ambalo lilifanya mashambulizi kadhaa nchini Syria katika miaka ya karibuni. Ni nadra kwa Israel kukiri kufanya mashambulizi lakini imesema hatua zake huko Syria zinalenga majeshi yanayo ungwa mkono na Iran. Shambulizi la anga la mwezi Februari 2023 limepiga ujirani ule ule kama ilivyokuwa kwa shambulizi la Jumatano, lililouwa wataalam wa kijeshi kadhaa wa Iran. - VOA, AP, AFP, Reuters #Haifa ⁣⁣⁣⁣⁣#waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #shirikalamwezimwekundu⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣ #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #wahouthi #marekani #uingereza #shambulizi #dhamar #yemen #iran #syria.