Shehena ya kwanza ya chanjo za COVID-19 yawasili nchini

  • | Citizen TV
    Shehena ya kwanza ya chanjo za corona hatimaye iliwasili nchini jana usiku huku serikali ikielezea matumaini ya chanjo hizi katika kudhibiti kusambaa kwa tandavu hii. Waziri wa afya Mutahi Kagwe aliongoza ujumbe wa serikali kupokea shehena hiyo ya dozi zaidi ya milioni moja.